Featured Kimataifa

ABIRIA 49 WAHOFIWA KUFARIKI AJALI YA NDEGE URUSI

Written by mzalendoeditor

Ndege ya abiria ya Antonov An-24 inayomilikiwa na shirika la ndege la Angara, imeanguka katika eneo la Amur, mashariki mwa Urusi karibu na mpaka wa China, ikiwa na watu 49 ndani wakiwemo watoto watano na wafanyakazi sita wa ndege.

Kwa mujibu wa shirika la habari la TASS, wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo wanahofiwa kupoteza maisha. Ndege hiyo ilikuwa ikielekea mji wa Tynda na ilipotea kwenye rada wakati ikikaribia kutua.

Mamlaka ya dharura nchini Urusi imethibitisha kuwa mabaki ya ndege hiyo yameonekana yakiwa yanawaka moto kupitia helikopta ya uokoaji aina ya Mi-8, inayomilikiwa na mamlaka ya usafiri wa anga ya kiraia (Rosaviatsiya).

Ripoti za awali zinaeleza kuwa makosa ya rubani wakati wa kutua katika hali ya hewa yenye uoni hafifu huenda ndiyo sababu ya ajali hiyo. Ndege hiyo, aina ya An-24, ni ya zamani na ilitengenezwa tangu miaka ya 1950, ikiwa bado inatumika Urusi kwa usafiri wa mizigo na abiria.

About the author

mzalendoeditor