Featured Kitaifa

KONGAMANO LA SEKTA YA MIFUGO: SERIKALI,BENKI YA EQUITY NA WADAU WAJADILI FURSA NA CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI 

Written by mzalendoeditor

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Edwin Mhede,akizungumza wakati akifungua  kongamano la ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za minyororo ya thamani ya mifugo na ngozi nchini Tanzania lililoandaliwa na Benki ya Equity lililofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dodoma.

 

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Edwin Mhede,akizungumza wakati akifungua   kongamano la ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za minyororo ya thamani ya mifugo na ngozi nchini Tanzania lililoandaliwa na Benki ya Equity lililofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Equity,Dkt.Florens Turuka,akizungumza wakati wa  kongamano la ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za minyororo ya thamani ya mifugo na ngozi nchini Tanzania lililoandaliwa na Benki ya Equity lililofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity,Isabela Maganga,akizungumza wakati wa  kongamano la ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za minyororo ya thamani ya mifugo na ngozi nchini Tanzania lililoandaliwa na Benki ya Equity lililofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa  kongamano la ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za minyororo ya thamani ya mifugo na ngozi nchini Tanzania lililoandaliwa na Benki ya Equity lililofanyika leo Julai 23,2025 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna – DODOMA

SERIKALI  imeitaka Benki ya Equity na Bodi yake kuunda timu ndogo itakayojumuisha wawakilishi kutoka serikalini na benki hiyo, kwa lengo la kusimamia mchakato wa uwekezaji katika sekta ya ngozi, hatua inayolenga kuinua hali ya kiuchumi ya wafugaji nchini.

Hayo yamesemwa leo Julai 23,2025 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt.Edwin Mhede,katika kongamano la ngazi ya juu kuhusu kufungua fursa za minyororo ya thamani ya mifugo na ngozi nchini Tanzania lililoandaliwa na Benki ya Equity.

Dkt. Mhede amesema kuwa  timu hiyo itasaidia kuhakikisha wawekezaji na wazalishaji wakubwa wa ngozi nchini wananufaika na biashara hiyo huku wakiliinua taifa kiuchumi. Ameongeza kuwa mafanikio ya sekta hiyo yatategemea ushirikiano wa karibu baina ya wadau na kuepuka ubinafsi.

“Nawapongeza sana Equity Benki kwa kuonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya ngozi. Naomba mshirikiane na wadau wengine ili mfanikishe kile mlichokusudia,” amesema Dkt. Mhede.

Aidha, ameeleza kuwa hadi kufikia jana, serikali imefanikiwa kuchanja mifugo milioni 16 katika maeneo mbalimbali nchini na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa wafugaji kuchanja mifugo yao ili kupata ngozi bora kwa ajili ya biashara ndani na nje ya nchi.

Dkt. Mhede,ameipongeza Benki ya Equity  kwa kuandaa kongamano hilo muhimu, na kuonesha utayari wa kushirikiana na serikali katika kuwezesha mitaji, kuboresha biashara za wafugaji, pamoja na kuimarisha minyororo ya thamani katika sekta ya mifugo.

“Kongamano hili ni fursa ya kipekee ya kufanya tathmini ya kina kuhusu hali ya sekta ya mifugo. Kupitia jukwaa hili, tunaweza kuona fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili sekta, ili kwa pamoja tuweze kuchukua hatua sahihi za maendeleo,” ameeleza 

Pia amesisitiza kuwa sekta ya mifugo ni uti wa mgongo kwa mamilioni ya Watanzania, hivyo ushirikiano wa karibu na taasisi kama Benki ya  Equity  ni msingi imara wa mageuzi chanya katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Dkt. Mhede,ametoa wito kwa wadau wengine kutoka sekta mbalimbali kuiga mfano wa Benki ya Equity  kwa kuwekeza katika sekta ya mifugo, kwa kuwa ina fursa nyingi ambazo hazijatumika kikamilifu, hasa kwenye maeneo ya uzalishaji wa ngozi, usindikaji wa mazao ya mifugo, na upatikanaji wa masoko ya uhakika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Equity,Dkt.Florens Turuka, amesema kuwa benki hiyo imeona fursa nyingi katika sekta ya ngozi, hali iliyowasukuma kuwekeza moja kwa moja katika sekta hiyo ili kusaidia wafugaji kufikia maendeleo.

“Fursa zilizopo kwenye sekta ndogo ya ngozi ni nyingi sana, hivyo wafugaji wanapaswa kujitokeza kushirikiana nasi ili waendelee kukuza biashara yao,” amesema Dkt. Turuka.

Naye , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity,Isabela Maganga,amesema kuwa benki hiyo imejipanga kushirikiana na serikali katika kuwekeza kwenye sekta ya mifugo, hasa zao la ngozi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupanua wigo wa biashara na kusaidia wananchi.

“Kama benki, tumejipanga kuhakikisha sekta ya ngozi inakua. Tumeamua kuwekeza kwa sababu tunatambua fursa lukuki zilizopo na tunataka kugusa maisha ya wananchi,” amesema Maganga.

Aidha amewataka wafugaji kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa na benki hiyo ili waweze kupiga hatua katika biashara ya ngozi wanayofanya kwenye maeneo mbalimbali nchini.

About the author

mzalendoeditor