Featured Kitaifa

DKT. HUSSEIN OMAR ATOA MAELEKEZO TET KUIMARISHA MATUMIZI YA TEHAMA

Written by mzalendoeditor


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Mohamed Omar, ameitaka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili mitaala na vitabu viweze kuwafikia walimu na wanafunzi wengi na kwa urahisi.

Akiwa katika ziara yake Julai 22, 2025, alisisitiza pia umuhimu wa kutumia TEHAMA hususan katika maeneo yenye upungufu wa walimu, ili kuondoa pengo la kitaaluma katika mazingira hayo.

Aidha, Dkt. Hussein alielekeza TET kutumia maboresho ya Mtaala wa Elimu ya Amali kama nyenzo ya kukabiliana na changamoto za kijamii na kutoa wito kwa taasisi hiyo kuandaa mtaala mahsusi wa kushughulikia changamoto ya taka ngumu mijini, kwa kuzingatia ujuzi wa vitendo unaohitajika katika soko la sasa.

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba, alisema taasisi iko katika hatua za kufanya utafiti na kufuatilia utekelezaji wa mitaala mipya ili kuhakikisha inaleta mayokeo chanya ya kielimu












About the author

mzalendoeditor