Featured Kitaifa

SUDAN KUSINI WAJA TANZANIA KUJIFUNZA MAGEUZI YA ELIMU

Written by mzalendoeditor

Hatua ya Mageuzi ya Elimu Tanzania imeendelea kuwa kuvutia nchi mbalimbali za Afrika kujifunza ikiwemo uboreshaji Sera na mabadiliko ya Mtaala katika ngazi mbalimbali za elimu.

Juali 18, Viongozi kutoka Wizara ya Elimu Sudan Kusini wakiongozwa hiyo.Mhe. Kacuol Mabil Piok wamekutana na Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Kibaha Mkoani Pwani chini ya Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo wakiwa katika ziara maalum ya kujifunza utekelezaji mageuzi ya kielimu.

Sudan Kusini imevutiwa na jinsi Tanzania inavyotekeleza afua mbali za kielimu ikiwemo uwekezaji rasimali katika sekta kwa ujumla na miradi ya elimu ikiwemo utekelezaji mpango wa elimu nje ya mfumo rasmi ambapo Mhe Piok amesema wamevutiwa sana na maendeleo na Elimu Tanzania na hivyo kuamua kuja kujifunza na kuanzisha ushirikiano ili kuendelea kubadilishana uzoefu kama Nchi za Afrika Mashariki.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu Prof Nombo amewashukuru kwa kutambua Maendeleo ya Elimu Tanzania na kuamua kuja kujifunza, aidha ameongeza kuwa Wizara ya Elimu inaendelea kupokea nchi mbalimbali kuja kujifunza mageuzi ya elimu ambayo yanalenga kuandaa wahitmu wenye maarifa na ujuzi.

About the author

mzalendoeditor