Na. Jeshi la Polisi,DODOMA
Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, akimpitisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akiwa ameambatana na Makamishna wengine kwenye maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari unaoendelea Mkoani Dodoma.
Mpaka sasa jumla ya maghorofa sita yanajengwa kwa pamoja ambapo ujenzi huo umefikia katika hatua mbalimbali huku kila ghorofa moja ikiwa na sakafu (floor) nne.
Tukio hilo limefanyika leo Julai 15,2025 wakati Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, akifanya ukaguzi wa majenzi unaoendelea mkoani humo.
Akihitimisha ukaguzi huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, kwa mara nyingine ameendelea kutoa shukurani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa jinsi anavyoendelea kuboresha Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ofisi, vyuo vya Polisi na makazi ya askari kama haya yanayoendelea kujengwa mkoani Dodoma.