Featured Kitaifa

TANZANIA YAENDELEA KUFANYA VIZURI  MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene akizungumza leo Julia 11,2025 jijini Dodoma ,wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Chrispin Chalamila,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika,Benjamin Kapera,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA) Bw.Ali Abdalla Ali,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali katika  Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali katika  Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali katika  Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Palamagamba Kabudi,akitoa mada wakati wa  Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika,yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais –Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene,amesema Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa kila mwaka  kutokana na utawala bora uliopo hapa nchini.
Waziri Simbachawene ameyasema hayowakati akifungua Kongamano la maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika yaliyofanyika leo Julai 11,2025 jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yakiongozwa na kauli mbiu ya kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya rushwa, ikizikumbusha taasisi zinazoratibu mapambano dhidi ya rushwa katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kulinda utu na haki za kila mtu ili kuimarisha utawala bora.
Amesema kuanzishwa kwa Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ndani ya Mahakama Kuu pamoja na Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 ni hatua nyingine muhimu katika kuhakikisha kwamba vitendo vya rushwa vinadhibitiwa ipasavyo.
 “Tanzania imepiga hatua kubwa katika jitihada za kutokomeza rushwa, ikiwa ni pamoja na kutunga na kufanya maboresho ya sheria mbalimbali zinazolenga kupambana na vitendo hivyo.”amesema Waziri Simbachawene
Aidha ameielekeza Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.
“Natoa wito kwa wadau wote kuja na mbinu mpya ambazo hazijazoeleka ili kusaidia kuboresha mapambano dhidi ya rushwa. Tunapaswa kuangalia namna taasisi zetu zinavyohudumia wananchi, kwani huduma bora na haki ni kipimo muhimu cha mafanikio yetu,” amesema  Simbachawene.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Chrispin Chalamila,amesema kuwa rushwa ni kikwazo kikubwa kwa ustawi wa wananchi na inachangia kuwepo kwa vitendo vingine vya kidhalimu ambavyo vimekatazwa katika katiba ya Tanzania.
Bw.Chalamila amesema kuwa jitihada za kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya Vitendo vya rushwa zitachangia kufikia lengo la Serikali la kuleta ustawi wa jamii ya watanzania na kukuza heshima ya ubinadamu.
“Majadiliano kuhusu rushwa yanayofanyika katika maadhimishoo hayo yatasaidia kukuza heshima ya binadamu barani Afrika,ambapo mara nyingi huchukuliwa haki zao kutokana na vitendo vya rushwa”ameongeza
Naye Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA) Bw.Ali Abdalla Ali,ameseam kuwa maadhimisho hayo yatasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi nchini.
“Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya rushwa,ikizikumbusha taasisi zinazoratibu mapambano dhidi ya rushwa katika nchi wanachama wa umoja wa Afrika kulinda utu na haki za kila mtu ili kuimarisha utawala bora”amesema Bw.Ali
Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika,Benjamin Kapera,ametoa wito kwa Serikali za Afrika kuwekeza katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuhakikisha uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa usawa.
akitoa mada katika Kongamano hilo,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Palamagamba Kabudi amesisitiza umuhimu wa heshima ya binadamu kama haki ya msingi inayotambuliwa na mikataba ya kimataifa pamoja na katiba ya nchi.
Amesema kuwa uwepo wa rushwa katika jamii unavuruga misingi ya haki,usawa na utu wa binadamu na kwamba rushwa inapozidi watu hukosa huduma zinazostahili.
“ILi kukuza na kulinda heshima ya binadamu,ni muhimu kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa njia madhubuti,shirikishi na endelevu”amesisitiza

About the author

mzalendoeditor