Featured Kitaifa

ELON MUSK AZINDUA CHAMA KIPYA CHA KISIASA MAREKANI

Written by mzalendoeditor

Elon Musk, mshirika wa zamani wa Rais wa Marekani Donald Trump, jana Jumamosi alizindua chama kipya cha kisiasa nchini Marekani. Hatua hiyo inalenga kupinga kile alichokitaja kuwa “mfumo wa chama kimoja.”

Elon Musk, mfanyabiashara maarufu na mshirika wa zamani wa Rais wa Marekani Donald Trump, jana Jumamosi alizindua chama kipya cha kisiasa nchini Marekani.

Hatua hiyo inalenga kupinga kile alichokitaja kuwa “mfumo wa chama kimoja” unaodhoofisha demokrasia nchini humo.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Musk aliandika: “Linapokuja suala la kufilisi nchi yetu kupitia ubadhirifu na ufisadi, tunaishi ndani ya mfumo wa chama kimoja  siyo demokrasia.” Bilionea huyo ametangaza kuanzisha chama kipya kiitwacho “American Party”, ambacho amesema kitaongoza juhudi za kurekebisha mfumo wa sasa wa kisiasa.Musk, ambaye ni mmoja wa watu matajiri zaidi duniani na alikuwa mfadhili mkubwa wa kampeni ya Trump kwa uchaguzi wa 2024, aliingia katika mvutano mkubwa na rais huyo, baada ya Musk kuongoza jitihada za Chama cha Republican kupunguza matumizi ya serikali na kupunguza ukubwa wa utawala wa shirikisho alipokuwa akiongoza Idara ya Ufanisi Serikalini (DOGE).

Tofauti zao zilijikita zaidi katika mpango wa matumizi makubwa ya ndani uliopendekezwa na Trump, ambao Musk aliupinga vikali. Alionya kuwa mpango huo unaweza kulipua deni la taifa, na akaahidi kutumia ushawishi wake wa kisiasa kuwazuia wabunge wanaounga mkono pendekezo hilo.

Chanzo:Dw kiswahili

About the author

mzalendoeditor