Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA UPADIRISHO JIMBO KATOLIKI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapongeza Mapadre wapya waliopata daraja la Upadre katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 05 Julai 2025.

….

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki kushiriki katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. 

Misa hiyo Takatifu imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkna kuongozwa na ime Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya. 

Askofu Kinyaiya amewasisitiza waumini kujitokeza katika kupiga kura kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu watakaowatumikia kwa miaka mitano ijayo. Pia ametoa rai ya matumizi sahihi ya akili mnemba (AI) ili kuepusha maovu na udanganyifu katika jamii.

Jumla ya Mashemasi watatu wamepata daraja la Upadre katika Misa hiyo ambao ni Padre Joseph Ibrahim, Padre Sajilo Mark pamoja Padre Damian Mtanduzi.

Aidha Misa hiyo imeambatana na uwekaji wa Jiwe la Msingi ujenzi wa jengo la Katekesi (Jengo la kufundishia dini) lililopo katika Parokia hiyo ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya wakati akiwasili Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma kushiriki Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia hiyo. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma kushiriki Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia hiyo. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya wakiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Katekesi (Jengo la kufundishia dini) lililopo katika Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma wakati wa Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia hiyo. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapongeza Mapadre wapya waliopata daraja la Upadre katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya, Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi, Mapadre pamoja na Mapadre wapya waliopata daraja la Upadre katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya, Askofu Msaidizi Wilbroad Kibozi, Mapadre pamoja na  Mapadre wapya waliopata daraja la Upadre wakirusha njiwa kuashiria kuanza kwa jubilee ya miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege mara baada ya Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 05 Julai 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipanda mti wakati wa sherehe za ufunguzi wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege mara baada ya Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma. Tarehe 05 Julai 2025.

About the author

mzalendoeditor