Featured Kitaifa

WAZABUNI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA MAONESHO YA SABASABA KUPATA TAARIFA

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe (kulia), akimsikiliza Afisa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bi. Eva Valerian, kuhusu matoleo mbalimbali ya Jarida la Wizara ya Fedha maarufu kama Hazina Yetu pamoja na namna wanavyohabarisha umma kupitia mitandao ya kijamii, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi , WF, Dar es Salaam
Wazabuni wanaotaka kufanya kazi na Wizara, Taasisi na Mashirika ya Umma  wametakiwa kufahamu Sera, Sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ili kuweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi. 
Hayo yamesemwa na Kamishna wa  Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga  alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na mabanda mengine kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya TANTRADE, Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Idara yake ndiyo yenye jukumu la kuandaa Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, kanuni na miongozo inayolenga kukuza ushiriki wa wajasiriamali wadogo na wakati katika masoko ya ununuzi na ugavi katika sekta ya umma.
Dkt. Mwakibinga ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa ya Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam kupata taarifa sahihi kuhusu Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ili waweze kushiriki katika zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Serikali.
Alisema kuwa ni vigumu kupata taarifa nyingi kwa pamoja lakini kupitia Maonesho hayo, mwananchi anaweza kupata taarifa kikamilifu kupitia Idara, Vitengo na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha ambazo zinahusika katika masuala ya Ununuzi wa Umma na Ugavi.
Alisema katika Banda la Wizara ya Fedha ipo Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ambazo zote zinahusika katika masuala mbalimbali kuhusiana na ununuzi wa umma na ugavi.
Alisema kazi kubwa inayofanywa na Idara yake ni kutengeneza mazingira mazuri katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi kupitia Sera ili wananchi wengi waweze kunufaika na mazingira hayo.
Dkt. Mwakibinga amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali likiwemo banda la Shirika la Bima la Taifa (NIC), Shirika la Mawasiliano la Vodacom, Lazziz Bakery, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bodi ya Bima ya Amana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.  
Aidha, alisema kuwa Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Sabasaba limesheheni wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Wizara hiyo na Taasisi zake ikiwa ni pamoja na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT AMIS), Mfuko wa Self Microfinance, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
Taasisi nyingine ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Benki ya Maendeleo TIB na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hazina SACCOS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Dkt. Fredereck Mwakibinga, akisaini kitabu cha wageni wakati aliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” yanayoendelea katika Viwanja vya TANTRADE Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe (kulia), akimsikiliza Afisa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bi. Eva Valerian, kuhusu matoleo mbalimbali ya Jarida la Wizara ya Fedha maarufu kama Hazina Yetu pamoja na namna wanavyohabarisha umma kupitia mitandao ya kijamii, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha, Dkt. Fredereck Mwakibinga (kushoto), akisoma moja ya chapisho la Taasisi ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), alilokabidhiwa na maafisa wa Taasisi hiyo (kulia), wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Kilindomo (Kulia), akimwonesha Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Bw. Omari Abdallah (kushoto), Kitabu cha Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe (kulia), akimsikiliza  Afisa Sheria Mkuu wa Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (ToST), Wakili Aderickson Njunwa (kushoto), kuhusu namna wanavyoshughulikia malalamiko ya Kodi na kusuluhisha, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Mchumi Mwandamizi kutoka Idara ya Bajeti, Bw. Samweli Mkwama (Kulia), akimwelezea Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Bi. Nadia Ally (kushoto), kuhusu masuala mbalimbali ya uandaaji wa Bajeti, pindi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu. Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Kilindomo.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha, Dkt. Fredereck Mwakibinga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, na Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma, pindi alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yenye kaulimbiu ya “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania” ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu. 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

About the author

mzalendoeditor