Featured Kitaifa

FCC KUTUMIA FURSA YA MAONESHO YA 49 SABASABA KUTOA ELIMU KWA UMMA

Written by mzalendoeditor

πŸ“Dar es SalaamΒ 

Tume ya Ushindani (FCC), imeendelea kutumia fursa ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kwa kutoa elimu kwa Umma ambao ndio walaji au watumiaji wa bidhaa na huduma.Β 

Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania”, yameanza tarehe 28 Juni na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai, 2025.Β 

Wananchi mbalimbali wameendelea kujitokeza na kutembelea banda la FCC ambapo wamenufaika kwa kupata elimu zaidi inayohusu masuala ya Ushindani, Udhibiti wa Bidhaa Bandia na Kumlinda Mlaji kutoka kwa watumishi wa FCC.

About the author

mzalendoeditor