Featured Kitaifa

DKT.MADELE AREJESHA FOMU YA UBUNGE DODOMA MJINI

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna-DODOMA

AFISA  Mwanadamizi Ofisi ya Rais Ikulu, Dk Fabian Madele,amerejesha fomu  ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Dodoma Mjini.

Dkt.Madele amerejesha fomu hiyo  kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini  Bi.Sophia Kibaba,mapema leo Julai 1,2025.
Zoezi la uchukuaji fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.

About the author

mzalendoeditor