Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini, Sandro Agostinho de Oliveira, Juni 28, 2025 jijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa amekutana na kumuaga balozi de Oliveira kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
*Ampongeza kwa kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini.
* Balozi de Oliveira asema Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Juni 28, 2025 amemuaga rasmi Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro Agostinho de Oliveira, ambaye anamaliza muda wake wa uwakilishi baada ya kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye ameagana na Balozi huyo jijini Dodoma kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu, amempongeza Balozi de Oliveira kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kisiasa na kijamii kati ya Tanzania na Angola.
Mheshimiwa Majaliwa amemweleza balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuthamini na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na kidugu kati ya Tanzania na Angola katika nyanja zote muhimu za maendeleo.
Balozi de Oliveira ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote wa uwakilishi wake na amesema kuwa Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania katika kuendeleza ustawi wa nchi hizo mbili.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini, Sandro Agostinho de Oliveira, Juni 28, 2025 jijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa amekutana na kumuaga balozi de Oliveira kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini, Sandro Agostinho de Oliveira, Juni 28, 2025 jijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa amekutana na kumuaga balozi de Oliveira kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)