Featured Kitaifa

KISARO ALITAKA JIMBO LA DODOMA MJINI

Written by mzalendoeditor

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini,Samuel Kisaro amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Kisaro ambaye ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Dodoma Mjini amechukua fomu hiyo Leo Juni 28 katika ofisi ya CCM Wilaya ya Dodoma Mjini ambapo emekabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Sophia Kibaba.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu,Kisaro,amejitokeza kuchukua fomu ikiwa ni kutumia haki yake ya kikatiba kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Dodoma Mjini.

“Nimepokea fomu nipo tayari kuijaza kwa ajili ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,”

“Nimekuwa na dhamira ya dhati kutoka moyoni mwangu niichukue fomi ili panapo majaliwa nikipata nafasi niwatumikie wananchi wa Dodoma Mjini kwa nafasi ya ubunge.”amesema Kisaro

About the author

mzalendoeditor