Featured Kitaifa

DKT.MADELE AUTAKA UBUNGE DODOMA MJINI

Written by mzalendoeditor

LEO Juni 28,2025 wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameaza kujitokeza kuchukua fomu kuomba idhini ya kuwania nafasi ya ubunge na udiwani katika majimbo ya Dodoma Mjini na Jimbo la Mtumba.
Akizungumza mara ya kuchukua fomu, Dk Fabian Madele ambaye mshauri wa Rais alisema amejitokeza kuchukua fomu ikiwa ni kutumia haki yake ya kikatiba kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Dodoma Mjini.
“Leo nimetumia haki yangu ya kikatiba kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi kwa Jimbo la Dodoma Mjini”
“Nimekuwa na dhamira ya dhati kutoka mourning mwangu niichukue fomi ili panapo majaliwa nikipata nafasi niwatumikie wananchi wa Dodoma Mjini kwa nafasi ya ubunge.”

About the author

mzalendoeditor