π Pamoja na kuimarisha afya za Watumishi; Linalenga kuhamasisha ushiriki wa Uchaguzi Mkuu 2025
π Ni la pili kufanyika tangu kuasisiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katikaΒ Bonanza la Wizara ya Nishati na Taasisi zake litakalofanyika jumamosi JuniΒ 28, 2025Β jijini Dodoma.
Akizungumzia maandalizi ya BonanzaΒ hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati, Bi. Neema Mbuja amesema kuwa, Nishati Bonanza litafanyika kwenye Viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma na kushirikisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na wadau kutoka Wizara nyingine.
ββ Nipende kuchukua fursa hii kuzikaribisha taasisi zilizo chini yaΒ Wizara ya NishatiΒ kushiriki kikamilifuΒ bonanza ambalo linaleta fursa ya kufahamiana na kubadilishana mawazo baada ya muda wa kazi pamoja naΒ kufanya mazoezi ili kujenga afya.” Amesema Mbuja
Ameongeza kuwa, kwaΒ mwaka huu Nishati BonanzaΒ linaongozwa na kauli mbiu ya “Michezo kwa Afya bora, Shiriki uchaguzi 2025 ikiwa na lengo pia la kuhamasisha wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 .
Amesema maandalizi yote yameshakamilika na timu zitakazoshiriki michezo mbalimbali zimeshawasili Dodoma kushiriki bonanza hilo litakaloshirikisha watu takribani 1000.
Ametaja michezo itakayoshindaniwa kuwa niΒ ni pamoja na Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Kuvuta Kamba, pamoja naΒ michezo ya jadi kama vile bao na drafti, piaΒ Β kufukuza kuku.
Taasisi zitakazoshiriki Bonanza hilo laΒ Nishati ni pamoja na TANESCO, REA, TPDC, PURA, EWURA, TGDC, ETDCO, TCPM, TANOIL, GASCO, PBPA.
Hili ni Bonanza la pili kufanyika tangu kuasisiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Β Dkt Doto Biteko mwaka jana.







