Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,Dkt Franklin Jasson Rwezimula ametoa wito kwa Watumishi Tume ya Haki na Utawala Bora kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ili wapate haki zao.
Dkt Rwezimula ametoa wito huo Juni 23,2023 wakati alipotembelea Banda la THBUB katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Dkt.amesema kuwa wananchi wanapopata changamoto ya haki za binadamu na utawala bora wanaamini kuwa hapa ni mahala sahihi kwa kupata haki zao
“Hivyo nanyi mshughulikie malalamiko yao kwa ueledi na ufanisi ili wapate haki zao”amesema Dkt. Rwezimula
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalifunguliwa Juni 16,2025 ikiwa na lengo kuwahudumia Watumishi wa Umma na Wananchi kwa pamoja.