Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, kuhusu huduma zinazotolewa katika Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akiagana na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Stellah Mtally, akitoa elimu kuhusu Pensheni inayolipwa na Hazina kwa Wastaafu kwa Mkazi wa Dodoma Bw. Michael Mshana, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Taifa, Boniface Kilindimo, akitoa elimu kuhusu maandalizi ya bajeti ya Serikali na Usimamizi wake kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bw. Raphael Macha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Mtumishi wa Hazina Saccos, Bi. Leah Nkinda, akieleza hatua za kujiunga na Saccos hiyo na faida zake kwa Bi. Doroth Mayala, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. William Marwa, akitoa elimu ya namna ya uondoshaji wa mali chakavu kwa watumishi wa umma waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Grace Samwel, akitoa elimu ya uwekezaji kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bw. Raphael Macha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Maafisa kutoka Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Naibu Waziri wa Ofi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutoa elimu kwa weledi kwa wananchi.
Pongezi hizo amezitoa alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma kuanzia Juni 16 hadi 23 mwaka huu.
Amesema kuwa elimu kuhusu masuala ya Bajeti, Usimamizi wa Mali za Serikali, , Usimamizi wa Deni la Taifa, Mifumo ya Fedha na Pensheni inayotolewa na Hazina kwa Wastaafu ni muhimu kwa wananchi wote wakiwemo watumishi wa umma.
Pongezi hizo zimetolewa baada ya kupata maelezo ya huduma zinazotolewa katika Wiki ya Utumishi wa Umma na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni.
Kwa upande mwingine, Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Stellah Mtally, amewataka wakazi wa Dodoma na maeneo mengine nchini kufahamu kuwa Ofisi ya Pensheni Hazina inajukumu la kulipa mafao ya kustaafu kwa viongozi wa kitaaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Bw. Mtally aliyasema hayo wakati akitoa elimu ya pesheni inayolipwa na Hazina kwa wastaafu kwa watu waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho hayo
Alisema kuwa aina za Mafao yanayotolewa na Ofisi ya Pensheni Hazina ni pamoja na Mafao ya Kiinua Mgongo yanayolipwa kwa mkupuo mmoja kwa mtumishi anapostaafu kwa mujibu wa Sheria.
Alitaja mafao mengine kuwa ni pamoja na Pensheni ya kila Mwezi anayolipwa mstaafu baada ya kustaafu, Mafao ya Mirathi, Pensheni ya Kifo, Mafao kwa Wategemezi wa marehemu ambaye alikuwa kwenye ajira ya masharti ya kudumu na malipo ya uzeeni, ambapo marehemu anatakiwa kuwa alifanya kazi muda usiopupungua miaka 15.
Aidha Bi. Mtally alisema pia kuna mafao ya pensheni ya ulemavu na mafao ya mkataba ambayo ndiyo kiinua mgongo.