Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI BUSEGA MKOANI SIMIYU

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Mradi wa Maji wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 12 katika Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu.

Mradi wa Lamadi ni sehemu ya mpango mkubwa wa Satellites Town Projects uliotekelezwa na Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) na kusimamiwa hivi sasa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Busega (BUSEWASA).

Sanjari na Lamadi, miji ya Magu na Misungwi imenufaika kupitia mpango huu unaolenga kuongeza kiwango cha huduma ya maji katika miji inayokua kwa kasi.

Kukamilika kwa Mradi huu kumeboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Kata ya Lamadi na vijiji vya jirani wapatao 85,000.

Upatikanaji wa maji kwa sasa katika Mji wa Lamadi umefikia asilimia 97 na kufanya lengo la Serikali la kufikia lengo la zaidi ya asilimia 95 ya upatikanaji wa maji safi na salama Mijini.

About the author

mzalendoeditor