Featured Kitaifa

EWURA YAONGEZA UELEWA KWA WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA LPG JIJINI ARUSHA

Written by mzalendoeditor
Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.
….
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) – Kanda ya Kaskazini, leo tarehe 19 Juni 2025, imeendesha semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) katika Jiji la Arusha.
Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Longidu, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaelimisha wadau kuhusu masuala ya usalama katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ubora na usalama unaotakiwa.
Aidha, Mhandisi. Longidu alibainisha kuwa EWURA inaendelea kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ambao unalenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Alisema mkakati huo ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira, na kupunguza utegemezi wa nishati chafu kama kuni na mkaa.
Mhandisi wa Petroli Magreth Mwita pia aliwaeleza washiriki utaratibu sahihi wa kupata leseni kwa ajili ya kusambaza au kuuza LPG, na  kuzingatia matakwa ya kisheria na ya kiufundi ili kuhakikisha usalama wa watumiaji na uendelevu wa biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa LPG, Bw. Amos Mwansumbule, alisema soko linaendelea kukua kwa kasi kutokana na ongezeko la uelewa na kuwataka wasambazaji na wauzaji kuzingatia miongozo ili biashara ya gesi isaidie kulinda mazingira na kuleta unafuu.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi. Lorivii Long’idu,akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.

Mhandisi wa Petroli Magreth Mwita,akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.

 

Sehemu ya washiriki wakifuatilia semina ya kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi. Lorivii Long’idu,(aliyekaa katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina ya  kuwajengea uwezo wasambazaji na wauzaji wa gesi ya kupikia (LPG) Jiji la Arusha.

About the author

mzalendoeditor