Na.Meleka Kulwa_DODOMA
Katika kuadhimisha siku ya Selimundu duniani Hospitali ya Benjamin Mkapa yafanikiwa kutibu watoto 21 wenye ugonjwa wa selimundu.
Hayo yamesemwa leo juni 19.2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Benjamini Prof.Abel Makubi wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya selimundu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Prof.Makubi amesema serikali inaendelea kuboresha sekta ya Afya ambapo mpaka sasa imetoa billion 1.7 kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wasiokuwa na uwezo kumudu gharama za matibabu ya selimundu.
“Huduma hizi ni gharama ambapo mgonjwa mmoja anatibiwa kwa zaidi ya million 70 hivyo niwakumbushe watanzania kujiunga na Bima ya Afya ili kuwe na unafuu wa gharama.”Amesema Prof Makubi.
Prof.Makubi amesema Hospitali ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na wizara ya Afya wamepanga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa selimundu na kuongeza Kasi ya kubaini wabebaji wa vinasaba kwa ajili ya selimundu ambavyo vitasaidia kuepukana na Ugonjwa huo.
“Nawashauri vijana wanaotarajia kuoana wapime kwanza vina Saba Ili kujua kama mmoja wapo anadalili za ugonjwa huo ili waweze kuepukana na ugonjwa wa selimundu.”Amesema Prof. Makubi.
Aidha amewataka watanzania kuendelea kuwapima watoto ili wanapobainika kuwa na ugonjwa huo waweze kutibiwa kwa haraka.
Kalisti Mayala ni mmoja wa watoto aliyetibiwa ambaye tayari amepona ameishukuru Serikali pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa Huduma nzuri aliyoipata tangu alipoingia hospitalini hapo.
Hata hivyo kwa upande wake Mama Israel mama wa watoto wawili waliokuwa na Sellimundu ameishukuru serikali kwa kuboresha huduma na amesema Kuna haja ya Elimu kutolewa kwa wingi ili jamii iepukane na Mila potofu kuwa ugonjwa wa selimundu hutokana na Imani za kishirikina.