Featured Kitaifa

RAIS SAMIA NA RAIS WA BENKI YA AfDB WATEMBELEA MIRADI YA KIMAENDELEO JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete maraa baada ya Kuwasili kugagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma(Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3)katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.

Na.Meleka Kulwa_DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kukamilika kwa miradi ya Barabara ya Mzunguko wa Nje (Outer Ring Road) na uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato utarahisisha usafirishaji wa mazao, pembejeo na bidhaa nyingine kwa gharama nafuu na kasi kubwa, hivyo ni jukumu la wananchi kujiandaa kuitumia kikamilifu kwa kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza kilimo cha kisasa, hasa cha zabibu na alizeti ili kuongeza tija na kipato.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Juni 14,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Nala mara baada ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na mradi wa ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Msalato.

Amesema kuwa miradi hiyo imelenga kuimarisha miundombinu, kukuza uchumi wa taifa, na kuongeza fursa za maendeleo kwa wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

” Niwaomba wananchi wa Nala kutumia fursa ya miradi hiyo kwa kupanda matunda ya zabibu na alizeti ili kupendezesha barabara hizo. Aidha, aliitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha miradi hiyo inajengwa kwa viwango vya juu.”amesema Mhe.Rais Samia 

Rais Samia pia alitangaza kuwa Barabara ya Mzunguko wa Dodoma itapewa jina la Dkt. Akinwumi Adesina kama ishara ya kutambua mchango wake kupitia Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Rais Dkt. Samia,amemshukuru  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, kwa ushirikiano na ufadhili uliotolewa na AfDB kwa miradi mbalimbali ya barabara nchini, ikiwemo ya Barabara ya Kabingo–Kasulu–Manyovu, Dodoma–Babati, Mnivata–Masasi, Sakina–Tengeru, ufadhili kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, pamoja na vipande viwili vya reli ya kisasa (SGR) inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.

Hata hivyo  Rais  Samia amezielekeza Wizara za Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kwa ubora unaotakiwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuitunza ipasavyo ili idumu kwa muda mrefu na kutoa tija iliyokusudiwa kwa Taifa.

 

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alieleza kuwa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato ni utekelezaji wa ndoto ya muda mrefu ya viongozi wa awamu zilizopita, ambayo sasa imeanza kutimia.

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, alieleza kuwa miradi hiyo itapunguza msongamano wa magari na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Aliongeza kuwa serikali inaendelea na mipango ya kujenga barabara za mabasi yaendayo kasi jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, alibainisha kuwa kutua kwa ndege ya majaribio katika Kiwanja cha Ndege cha Msalato ni hatua muhimu katika kuboresha sekta ya uchukuzi nchini.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina, alipongeza juhudi za serikali ya Tanzania katika kuimarisha miundombinu. Alieleza kufurahishwa na safari ya treni ya kisasa (SGR), ambayo alisafiri nayo kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, kama ishara ya maendeleo makubwa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete maraa baada ya Kuwasili kugagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma(Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3)katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja naRais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma(Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3)katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili Mtumba kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma (Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3) Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.

Muonekano wa Barabara ya Mzunguko ya Dodoma (Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3) Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.

About the author

mzalendoeditor