Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA KESHO JUNI 14.2025 JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule, akziungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2025 kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara kesho Juni 14,2025 jijini Dodoma ya kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule, akziungumza na waandishi wa habari leo Juni 13,2025 kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara kesho Juni 14,2025 jijini Dodoma ya kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa huo.
Na.Meleka Kulwa-DODOMA
RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya siku  moja jijini Dodoma ya kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mkoa huo.
Hayo yamesemwa leo Juni 13,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule wakati akziungumza na waandishi wa habari kuelekea katika ziara hiyo.
Bi.Senyamule amesema kuwa  Rais Samia atakagua  miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato ambacho Ujenzi wake umeghariimu Sh. Billion 359 na Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje kutoka Mtumba, Veyula  hadi Nala, mradi  huo wenye thamani ya Shilingi bilioni 221.
“Kesho Juni 14,2025  Rais Samia atafanya ziara ya kukagua miradi katika Mkoa wetu ambapo  ataambatana  na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mhe. Dkt. Akinwumi Adesina katika ziara hiyo”amesema Bi.Senyamule
Hata hivyo ameongeza kuwa mara baada ya  kukagua maendeleo ya miradi ya Mkoa wa Dodoma Mhe.Rais Samia atahitimisha ziara yake kwa kuzungumza na wananchi wa Nala.
Aidha amesema kuwa   Mkoa wa Dodoma una miradi  3,093 ya kimaendeleo iliyotekelezwa na Serikali ikiwa na  thamani ya zaidi ya Shilingi trilioni 10 katika kipindi kifupi cha uongozi wake.
Bi.Senyamule ametoa wito kwa  wananchi wa Dodoma  kujitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Rais  Samia na kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo. Tukio hili ni nafasi adhimu ya kuonyesha shukrani kwa maendeleo makubwa yanayoendelea kushuhudiwa katika Mkoa wa Dodoma, ikiwemo huduma bora za maji, afya, na elimu.

About the author

mzalendoeditor