Featured Kitaifa

MAONESHO YA NANE NANE 2025 KUFANYIKA KITAIFA DODOMA

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni 13,2025 jijini Dodoma wakati akizindua tovuti ya usajili wa washiriki wa maonesho na sikukuu ya wakulima nane nane inayotarajiwa kufanyika Kitaifa jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amezindua tovuti ya usajili wa washiriki wa maonesho na sikukuu ya wakulima nane nane huku akowakishauriwa  wadau wa kilimo kuanza kujisajili kwenye Tovuti kuanzia Juni 17 na  Mwisho wa usajili ni Julai 16 Mwaka huu.
Waziri  Bashe ameyasema hayo leo Juni 13 ,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari  kuhusiana na maonyesho hayo yanayotarajia kuanzia Agosti Mosi hadi Agosti 8,mwaka huu.
Aidha Waziri Bashe aamesema  kuwa lengo la tovuti hiyo ni kurahisisha usajili wa Wadau wa Kilimo wa ndani na nje ya nchi katika kuwasilisha maombi ya huduma ya Mabanda kwa ajili ya maonesho.
“Wizara inahamasisha ushiriki wa Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Dodoma,Singida na mingine ya karibu katika  Maonyeshi hayo wakiwemo wakulima na wafugaji.”amesema Waziri Bashe.
“Wengine ni  wavuvi ,wasindikaji wa mazao ya kilimo na mifugi na uvuvi,wauza Pembejeo za kilimo,Mifugo na uvuvi pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo,”
Hata hivyo amesema kuwa  maonesho ya Nanenane ni  ya Kitaifa na Kimataifa na hufanyika kuanzia Agosti Mosi ya Kila Mwaka hadi Agosti 8 katika Kanda nane za maonyesho za Kanda ya Kati Nzuguni Mkoani Dodoma,ikiwemo Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya kiwanja cha John Mwakangale.
Waziri Bashe ametaja kanda nyingine ni kanda ya Mashariki Morogoro kiwanja cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,  Kanda ya kusini Lindi Kiwanja cha Ngongongo, Kanda ya Ziwa Magharibi Mwanza Kiwanja cha  Nyamuhongiro,Kanda ya ziwa Mashariki Simiyu Kiwanja cha Nyakabindi,  Kanda ya kaskazini Arusha Kiwanja cha Themi na    kanda ya magharibi Tabora Kiwanja cha Fatma Mwasa.
Pia Waziri Bashe amesema kuwa Kaulimbiu ya Maonesho ya mwaka huu ni ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025,”.

About the author

mzalendoeditor