Featured Kitaifa

KAMPUNI ZA MBOLEA ZA TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MKATABA WA BIASHARA

Written by mzalendoeditor

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imesaini mikataba na Kampuni ya United Capital Fertilizer Zambia Limited (UCFL) ya nchini Zambia kwa ajili wa mauziano ya mbolea aina ya NPK 10:18:24, UREA na CAN. Hafla hiyo imefanyika tarehe 11 Juni 2025, katika Wizara ya Kilimo jijini Dodoma.

Utiaji saini wa makubaliano hayo ya kibiashara ni kati ya Bw. Samuel Mshote, Mkurugenzi Mkuu wa TFC na Bw. Huang Yaachi, Mkurugenzi Mtendaji wa UCFL ya Zambia ambapo ni ishara ya mwendelezo wa biashara ya uuzaji wa mbolea ya ruzuku baina ya Kampuni hizo mbili.

About the author

mzalendoeditor