WAZIRI wa Afya Mhe.Jenista Mhagama,akiwalisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2025 leo Juni 2,2025 bungeni Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kipindi cha Julai 2024 hadi Machi, 2025, Wizara imeendelea kuboresha mazingira ya kutolea huduma za afya kwa wananchi katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo vitanda vimeongezeka kutoka 145,374 hadi kufikia vitanda 153,683.
Hayo yameelezwa leo Juni 2,2025 na Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akiwaslisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jenista amesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi, 2025, Wizara imeendelea kuboresha mazingira ya kutolea huduma za afya kwa wananchi katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo vitanda vimeongezeka kutoka 145,374 hadi kufikia vitanda 153,683.
“Hivyo kufanya uwaino wa vitanda 2.1 kwa kila watu 1,000 ukilinganisha na Mwongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaoelekeza kuwa na uwiano wa vitanda 2.5 kwa kila watu 1,000,”amesema Waziri Mhagama
Aidha, kati ya vitanda 153,683 vitanda 49,285 vipo katika ngazi ya Hospitali, vitanda 30,937 (462 )5% (1,254), 13% (8,328 ) 83% (1,013) 8% (1,676 ) 13% (113) 1% Hospitali Vituo vya afya Zahanati Kliniki Maabara Binafsi Vituo Vinginevyo 55 vipo katika Vituo vya Afya, vitanda 71,102 vipo katika Zahanati na vitanda 2,359 vinapatikana katika kliniki na vituo vinginevyo nchini,