Featured Kitaifa

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YATANGAZA VIPAUMBELE VYA MAGEUZI KWENYE BAJETI YA 2025/2026

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Dorothy Gwajima,akiwasilisha leo Mei 27,2025 bungeni jijini Dodoma  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Maendeleo  ya Jamii,Jinsia,Wazee,Wanawake na Makundi Maalum imeliomba Bunge kuiidhinishia bajeti ya Sh  bilioni 76 katika mwaka wa fedha 2025-2026  yenye vipaumbele vitano.
Akiwasilisha  makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo jana bungeni,Waziri wa Wizara hiyo,Dkt Dorothy Gwajima amevitaja vipaumbele hivyo ni Kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa katika ngazi ya msingi,kuimarisha mazingira ya ushiriki na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.
Pia  Kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za ustawi na maendeleo ya jamii ikiwa pamoja na kukuza usawa wa kijinsia, kutokomeza vitendo vya ukatili, uwezeshaji wanawake kiuchumi na upatikanaji wa malezi bora katika familia.
Vipaumbele vingine ni  Kutambua, kuratibu maendeleo na ustawi Makundi Maalum wakiwemo watoto, wazee na wafanyabiashara ndogondogo,Kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.

About the author

mzalendoeditor