Featured Kitaifa

DAR ES SALAAM KINARA WATOTO WA MITAANI

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Dorothy Gwajima,akiwasilisha leo Mei 27,2025 bungeni jijini Dodoma  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Maendeleoya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum imesema  Mikoa inayoongoza kuwa na watoto wengi wanaoishi na kufanya kazi Mtaani ni Dar es Salaam,ikifuatiwa na Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa  leo Mei 27,2025 bungeni na Waziri wa Wizara hiyo,Dkt Dorothy Gwajima wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Ameitaja mikoa mingine ni Mwanza, Mbeya, Arusha na Iringa huku Mikoa inayoongoza kuchangia maeneo ya miji kuwa na watoto zaidi ni Kagera, Geita, Kigoma, Dodoma, Mwanza na Shinyanga. 
Vilevile, Wizara imeandaa Kanuni za Utendaji (Standard Operating Procedure – SOP) za namna ya kushughulikia changamoto za Watoto waishio na Kufanya Kazi Mtaani.

About the author

mzalendoeditor