Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Mei 23,2025 wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA katika mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha
Na Kadama Malunde – Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amefunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA mkoa wa Shinyanga yaliyoendeshwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima  kwa ufadhili wa KOICA, akisisitiza kuwa programu hiyo ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha vijana kujikwamua kimaisha na kuleta maendeleo kwa taifa.
IPOSA ni kifupi cha Integrated Programme for Out-of-School Adolescents, ikiwa ni mpango jumuishi wa kuwawezesha vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu (hasa wenye umri wa miaka 15 hadi 19) kwa kuwapatia elimu mbadala, stadi za maisha, ujuzi wa awali wa ufundi, na maarifa ya ujasiriamali.
Akizungumza leo Ijumaa, Mei 23, 2025, wakati akifunga mafunzo hayo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Macha amesema mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku 21 katika mikoa sita ikiwemo Shinyanga, yamelenga kuwaandaa walimu kuwasaidia vijana waliokosa elimu ya kawaida kwa kuwapa ujuzi wa maisha, ujasiriamali na ufundi wa awali.
“Ni matumaini yangu kuwa walimu mliopata maarifa na ujuzi zaidi katika mafunzo haya mtatoa mchango mkubwa katika kuwawezesha vijana wetu walio nje ya shule kuweza kujikwamua kimaisha mmoja mmoja, na kama jamii na taifa kwa ujumla,” amesema Mhe. Macha.
Mkuu huyo wa Mkoa pia amewapongeza na kuwashukuru wadau wa maendeleo akiwemo KOICA, UNICEF, Plan International na Care International kwa kufadhili na kuendeleza IPOSA katika mikoa 16 huku akitoa wito kwa wadau wengine kuisaidia programu hiyo ifikie mikoa 10 iliyosalia.
Mhe. Macha amesisitiza kuwa elimu ya amali inayotolewa kupitia IPOSA inahitajika kwa kiwango kikubwa, na kuwataka viongozi kusaidia vijana waliopitia mafunzo hayo kupata mikopo, ajira na zabuni za halmashauri kama njia ya kuimarisha uchumi wa vijana na jamii.
Aidha, ameagiza mamlaka za elimu kuingiza shughuli za elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi katika mipango yao ya bajeti ili kuhakikisha mradi huu haukomei tu kwenye ufadhili wa sasa.
“Tunapaswa kujipanga vizuri namna huduma hizi zitakavyoendelezwa baada ya muda wa miradi kwisha,” ameongeza Mhe. Macha.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ameishauri Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima  kuendelea kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kusaidia nchi kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hususan lengo namba 4 la elimu kwa wote bila ubaguzi.
Mhe. Macha amewataka walimu kuhakikisha wanatumia maarifa waliyojifunza kwa ufanisi mkubwa na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii, huku akitoa wito kwa jamii yote kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga.
Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima , Prof. Philipo Sanga amesema lengo la IPOSA ni kumjenga kijana mwenye stadi mbalimbali ili aweze kujitegemea na kuwa tegemeo kwa jamii.
 
“Tunawaomba viongozi na walimu muwe bega kwa bega na vijana hawa kuwasaidia kupunguza changamoto za ajira na utegemezi,” amesema Prof. Sanga.
Naye Kaimu Afisa Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Shinyanga, George Ogutu, amesema IPOSA itasaidia kupunguza vijana tegemezi katika jamii na kuwaandaa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Programu ya IPOSA inalenga kuwasaidia vijana waliokosa fursa ya kuendelea na shule waweze kuishi maisha bora, kuwa na mchango chanya kwa jamii zao na kujikwamua kiuchumi.
Malengo mahususi ya IPOSA ni pamoja na kutoa elimu ya msingi kwa vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa shule, kuwajengea stadi za maisha na tabia chanya za kijamii, kukuza ujuzi wa awali na ujasiriamali ili kuwawezesha kuanzisha shughuli za kujitegemea, kuwezesha ushiriki wa vijana katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kupunguza changamoto kama ajira hatarishi, mimba za utotoni, na matumizi ya dawa za kulevya.
Mradi wa IPOSA ni mfano bora wa ubunifu wa kielimu unaoendana na mahitaji halisi ya jamii, hasa kwa vijana waliokosa fursa za elimu ya kawaida. Kwa kutoa mchanganyiko wa elimu, ujuzi, na mafunzo ya maisha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Mei 23,2025 wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA yaliyofanyika kwa muda wa siku 21 katika mkoa wa Shinyanga- Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Mei 23,2025 wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA katika mkoa wa Shinyanga 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA katika mkoa wa Shinyanga 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Mei 23,2025 wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA katika mkoa wa Shinyanga 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Mei 23,2025 wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA katika mkoa wa Shinyanga 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza leo Mei 23,2025 wakati akifunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA katika mkoa wa Shinyanga 
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Prof. Philipo Sanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Mkurugenzi – Taaluma wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Sempeho Siafu akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Mkurugenzi – Taaluma wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Sempeho Siafu akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Bakari Kasinyo akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Kaimu Afisa Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Shinyanga, George Ogutu akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Kaimu Afisa Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Shinyanga, George Ogutu akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu na viongozi wa Mradi wa IPOSA
Mratibu Msaidizi – IPOSA, Mwl. Mwajuma Mohamed akitoa mada kuhusu Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na IPOSA