Featured Kitaifa

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAOMBA KUIDHINISHIWA BILIONI 359.98

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana,akiwasilisha leo Mei 19,2025 bungeni jijini Dodoma  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Na.Alex Sonna-DODOMA
Wizara ya Maliasili na Utalii imeliomba Bunge kuliidhinishia Sh bilioni 359.98 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2025-2026
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo Mei 19,2025 bungeni,Waziri wa Wizara hiyo,Balozi Dk Pindi Chana amesema fedha hizo Sh bilioni 254.23 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 105.749 ni za miradi ya maendeleo.

About the author

mzalendoeditor