Featured Kitaifa

RC SENYAMULE AZINDUA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA NYUKI DUNIANI

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule,akikagua mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma leo Mei 18,2025.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule,akizungumza leo Mei 18,2025  na wananchi wa Mkoa wa Dodoma  wakati akizindua  maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma.

SEHEMU ya Wananchi wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule (hayupo pichani) ,akizungumza  wakati akizindua  maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Mhe.Rosemary Senyamule,amezindua maonyesho ya maadhimisho ya siku ya nyuki duniani huku akisisitiza ulinzi wa maeneo ya misitu ili kulinda viumbe hai ikiwemo nyuki  kwa sababu wana manufaa makubwa kwa Taifa.

Akizungumza leo Mei 18,2025  mara baada ya kuzindua maadhimisho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park,jijini Dodoma Mhe.Senyamule amesema kuwa sekta ya nyuki inakabiliwa na changamoto ambazo zinatishia uendelevu sekta hiyo  na hivyo kuhatarisha uvunaji wa mazao ya nyuki kwa siku zijazo.

“Bado tunayo nafasi kubwa ya kukuza na kuendeleza sekta hii. Ni wazi bado tunayo nafasi ya kuhifadhi misitu katika ardhi za vijiji, halmashauri, Serikali Kuu na hifadhi za wanyamapori,”amesema Mhe.Senyamule

Hata hivyo amesema kuwa  uchomaji wa misitu  ambayo inafanya nyuki kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine na wakati mwingine inasababisha kuwapoteza iwapo wataungua na moto huo.

Aidha, Senyamule amesema kuwa  Mkoa wa Dodoma una zaidi ya mizinga 18,000 ya nyuki yenye uwezo wa kuzalisha lita za asali 135,000.
 “Kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na fursa zilizopo katika Mkoa wa Dodoma ambapo kuna zaidi ya hekta milioni moja za misitu zilizohifadhiwa ambazo zinaweza kutumika katika shughuli za ufugaji nyuki.”amesisitiza
Madhimisho ya Nyuki Duniani hufanyika Mei 20 na Mwaka huu Kitaifa yanatarajia kufanyika jijini Dodoma na Mgeni rasmi katika Kilele hicho ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa
Kwa upande wake  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba amesema kuwa maadhimisho hayo yanaadhimishwa mara sita nchini.
“Pamoja na kutambua umuhimu wa nyuki, maadhimisho haya yanatoa  nafasi kwa wananchi kutoka mikoa mbalimbal kujumuika kwa pamoja na kutambua fursa mbalimbali zilizomo kwenye sekta hii,”alisema.
Aidha amesema kuwa  maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata uelewa wa mafanikio mbalimbali yanayotokana na sekta ya nyuki.

About the author

mzalendoeditor