Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATAKA WATANZANIA KUWA WAZALENDO KWA KUBORESHA TAARIFA ZAO NA KUJIANDIKISHA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionyesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma.

Na.Kulwa Meleka-CHAMWINO
RAIS wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameboresha taarifa zake za mpiga kura katika Kijiji Chamwino Ikulu, huku akiwataka watanzania kuwa wazalendo kwa  kuchangamkia haki yao ya msingi ya kujiandikisha.
Uboreshaji wa taarifa za mpiga kura awamu ya pili  ulianza Mei 16,2025 na unatarajia kukamilika Mei 22,mwaka huu  ambapo  Rais Samia  amehakiki taarifa zake katika kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino Ikulu.
Rais Samia alifika saa 8.20 mchana na moja kwa moja alielekea katika kituo cha kupiga kura ambapo alitumia dakika 10.
Mara baada ya kumaliza kujiandikisha,Rais Samia alipata nafasi ya kuzungumza na Wananchi waliojitokeza ambapo amewataka kujitokeza kwa wingi katika kuboresha taarifa zao ili waweze kupata haki yao .
“Nimeona nijiunge  nanyi kama mnavyojua  mimi ni mkazi wa Chamwino huko nyuma nimepiga kura sehemu  nyingi.Nimekuja kurekebisha taarifa zangu huko nyuma nilikuwa nikijiandikisha na kupiga kura  Zanzibar mwaka huu inabidi nipige hapa Makao Makuu  ya Nchi na Serikali,”amesema Rais Samia.
Aidha,Rais Samia amesisitizia wananchi kujitokeza kupiga kura kwani huo ni mzunguko wa pili na wasipofanya hivyo watakuwa wamepoteza haki yao ya msingi.
“Niwaombe tuje tupige kura huu ni mzunguko wa pili tukikosa huko mbele huwezi kurudia ili turudishe Serikali.Nitumie fursa hii kuwashukuru nawaomba waiteni ambao hawajaja waje,”amesema Rais Samia.
“Kazi  inachangamoto  wastahimili wale wanakuja kujiandikisha  waendelee kadi zimepungua subiri.Nataka niwahakikishie  kwa mipango mizuri kila mwenye haki ya kuandikishwa ataandikishwa,”amesema  Rais Samia.
Rais Samia amesema : “Kutokujitokeza ni kukataa haki ya kikatiba suala unajiuliza wewe ni mzalendo wa aina gani?
Nenda kapige kura wewe ukitaaa wenzako wataenda kumweka wanaomtaka suala kubwa hapa ni uzalendo hii ni fursa kubwa ni  vyema kila mtanzania ajitokeze atumie nafasi hii,”amesema Rais Samia.
Kwa upande wake Afisa Mwandikishaji kutoka Majimbo ya Chamwino na Mvumi,Godfrey Mnyamale amesema wananchi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha ambapo malengo ni kuwaandikisha wananchi 280,000.
Hata hivyo ameongeza kuwa  zoezi hilo ni muhimu  kwa wale ambao waliokosa nafasi ya kujiandikisha awamu ya kwanza,pamoja na wale ambao wanataka  jkubotesha  taarifa pamoja na wale waliokosa sifa.
“Kama alivyosema Mheshimiwa Rais,niwaombe wananchi wa Majimbo haya ya Chamwino na Mvumi kutumia fursa hii,”amesema Mnyamale.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionyesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chamwino mara baada ya kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo Mei,17, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma.

About the author

mzalendoeditor