Wataalamu wa Sekta ya Maji wa Tanzania Bara wamewapitisha wenzao kutoka Zanzibar kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji na usafi wa mazingira.
Wataalamu hao wanatoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mafunzo yamefanyika katika ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba jijini Dodoma.
Lengo la mafunzo ni kujenga uelewa kuhusu namna sahihi ya uendeshaji na miongozo kuhusu usambazaji na usimamizi wa rasilimali za maji na usafi wa mazingira baada ya mabadiliko ya sera ya maji,2025.
Kupitia sera hiyo Wizara ya Maji.,Nishati na Madini Zanzibar inategemea kubadilisha jina na majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Maji na kuwa Idara ya Maendeleo ya Maji na Usafi wa Mazingira
ambayo itakuwa na mgawanyo kuhusu Usimamizi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira na Usimamizi wa Rasilimali za maji.
Mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ,Mkurugenzi Ifara ya Sera na Mipango Prosper Buchafwe ndc amebainisha mafanikio yaliyopatikana katika eneo la Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingra kwa Tanzania bara ni pamoja na kuongezeka kwa hali ya upatikanaji wa maji kwa asilimia 83 vijijini na mijini asilimia 91, ujenzi na ukamilishwaji wa miradi ya maji ya kimkakati pamoja na kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji.