Featured Kitaifa

VIWANDA NA BIASHARA YAWEKEZA KATIKA VIWANDA VINAVYOZALISHA VIDHAA KWA WINGI NCHINI

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA  ya Viwanda na Biashara  imeendelea kuhamasisha ujenzi na upanuzi wa viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo pamoja na vile vinavyozalisha bidhaa zinazohitajika kwa wingi nchini kama vile viwanda vya Saruji, Mbolea, kuunganisha Magari, Sukari, Mabati na Vioo kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wake na  kuzalisha ajira kukuza mauzo ya nje ya nchi.
Hayo yameelezwa leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma  na Waziri wa Wizara hiyo,Dkt.Selemani Jafo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi  ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jafo amesema Kupitia Jitihada hizo mchango wa Sekta ya Viwanda na Biashara pamoja na ukuaji wake umeendelea kuimarika katika uchumi.
Amesema mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2024 ulikuwa asilimia 7.3 ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2023.
Aidha, ukuaji wa Sekta ya Viwanda ulikuwa asilimia 4.8 mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 4.3 mwaka 2023 ambapo  Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2024 ulikuwa asilimia 8.6 ikilinganishwa na asilimia 8.4 mwaka 2023.
Vilevile kasi ya ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.8 mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2023. Ukuaji huo umechangiwa na uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara.

About the author

mzalendoeditor