Featured Kimataifa

WAZIRI MASAUNI AANZA ZIARA YA KIKAZI NORWAY

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) akizungumza na viongozi mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili nchini Norway, Mei 12, 2025. Kushoto kwake ni Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes.

Mwandishi Wetu

Norway

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameanza ziara ya siku tatu jijini Oslo, nchini Norway ikiwa na lengo la kujifunza njia za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Waziri Masauni amesema ziara hiyo imeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Norway kufutia mwaliko uliotolewa kwa Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo baada ya kuwasili alipokelewa na Mhe. Tone Tinnes, Balozi wa Norway nchini Tanzania Mei 12, 2025.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kupata uzoefu kuhusiana na masuala ya Mazingira, namna bora ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kupitia biashara ya Kaboni na teknolojia ya kutenganisha taka katika miji na kuzifanya kuwa fursa na hatimaye kuzaliwa bidhaa na malighafi zingine ikiwemo mbolea, Maji na nishati ya Umeme.

Katika ziara hiyo Mhe. Masauni atapata fursa ya kukutana na viongozi wa mbalimbali wa Serikali ya Norway akiwepo Waziri wa Hali ya Hewa na Mazingira wa Norway, Bw. Andreas Bjelland Eriksen, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bw. Asmund Aukrust, Mkurugenzi Mkuu wa Norad Bw. Bard Vegar Solhjell pamoja na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo endelevu (sustainable Development) katika Wizara ya Mamabo ya nchi za Nje ya Norway.

Katika ziara hiyo Mhe. Masauni pamoja na viongozi hao watapata fursa ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya Mazingira pamoja na ushirikiano katika jitihada ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Aidha, Mhe. Masauni atapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Manispaa ya Oslo, Hafslunf Celsio, pamoja na kampuni ya Equinor kwa lengo la kuona namna miji hiyo inavyofanya katika suala la mazingira.

Ujumbe wa Tanzania katika ziara hiyo umejumuisha Mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden, Mtaalaam kutoka kituo cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) na Wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes mara baada ya kuwasili nchini humo, Mei 12, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) akizungumza na viongozi mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili nchini Norway, Mei 12, 2025. Kushoto kwake ni Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akizungumza na viongozi mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili nchini Norway, Mei 12, 2025. Kushoto kwake ni Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes na kulia kwake ni Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Sweeden Bw. Abel Maganya.

About the author

mzalendoeditor