Featured Kitaifa

MADARASA 2730,MABWENI 140 KUJENGWA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda,akiwasilisha bungeni Jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026.

Na Alex Sonna,Dodoma

WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia itawezesha ujenzi wa madarasa 2,730 (shule za msingi 949 na sekondari 1,781) na mabweni 140 ili kuwezesha utekelezaji wa mpango wa elimu ya msingi ya lazima kwa miaka 10.
Hayo yameelezwa leo Mei 12,2025 bungeni na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026.
Prof Mkenda amesema  miundombinu bora ni muhimu katika kuboresha nakuimarisha
mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika
shule za msingi, sekondari na ualimu.
Amesema  kwa kutambua umuhimu huo Serikali itaendelea lkujenga na kukarabati miundombinu.
Amesema Wizara  itawezesha ujenzi wa madarasa 2,730 (shule za msingi 949 na sekondari 1,781)
na mabweni 140 ili kuwezesha utekelezaji
wa mpango wa elimu ya msingi ya lazima kwa miaka 10.

About the author

mzalendoeditor