Featured Kitaifa

IDADI YA WANUFAIKA WA MIKOPO YA JUU KUONGEZEKA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda,akiwasilisha leo Mei 12,2025 bungeni Jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026.

Na Alex Sonna,Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia itaendelea kutoa mikopo na ufadhili kwa wanafunzi wenye sifa ili kuongeza fursa za elimu ya juu nchini ambapo itaongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na
mikopo ya elimu ya juu kutoka 245,314 mwaka 2024/25 hadi wanafunzi 252,773 mwaka wa kwanza 88,320 na wanaoendelea
164,453) mwaka 2025/26.

Hayo yameelezwa leo bungeni,Mei 12,2025 na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hivyo kwa mwaka 2025-2026.

Prof Mkenda pia amesema Wizara itaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi
10,000 wa ngazi ya stashahada katika fani
87 za kipaumbele ikiwemo Sayansi, Teknolojia,
Uhandisi na Hisabati.

Vilevile itaendelea kutoa ufadhili kwa wanafunzi
2,630 wenye ufaulu wa juu katika masomo
ya sayansi kupitia SAMIA Skolashipu
ambapo kati ya hao wanafunzi wa mwaka
wa kwanza 1,220, shahada za umahiri 80
na wanafunzi wanaoendelea 1,330.

About the author

mzalendoeditor