Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dodoma,Ibrahim Sumbe,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Bonanza la Ushirika kuelekea Siku ya kuelekea Jukwa la Ushirika Mkoa wa Dodoma linalotarajia kufanyika Mei 15-16,mwaka huu katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Bonanza lililofanyika leo Mei 10,2025 katika Viwanja wa Kilimani Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MAADHIMISHO ya wiki ya Ushirika yamefunguliwa rasmi Jijini hapa kwa wanasaccos mbalimbali kushiriki michezo mbalimbali katika uwanja wa Kilimani Jijini hapa.
Akizungumza katika bonanza hilo katika uwanja wa Kilimani ,LeoMei 10,2025 Jijini hapa Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dodoma,Ibrahim Sumbe amesema Saccos mbalimbali zimeshiriki pamoja na familia zao kwa ajili ya kuweka miili vizuri na kujiandaa na wiki ya Jukwaa la Ushirika.
Amesema kuelekea maadhimisho ya mwaka huu wamejipanga ambapo kilele kitakuwa wiki ijayo.
Amesema Jumapili Mei 11,2025 watapeleka msaada katika hospitali ya Chamwino ambapo wamenunua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia watoto wachanga joto pamoja na mashuka na vitu vingine.
Amesema Alhamisi Mei 15 watakuwa na semina ya Saccos zote katika ukumbi wa Chimwaga pamoja na semina siku inayofuata na watakuwa na safari ya kuutangaza ushirika ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini,Anthony Mavunde.
Amesema siku ya Ijumaa watakuwa na safari ya kuendelea kuutangaza ushirika kwa ajili ya kwenda Arusha kutembelea mbuga za wanyama kwa kuangalia rasilimali za nchi.
“Tutaenda Ngorongoro kwa ajili ya kujionea mazuri ya Tanzania pamoja na kuutangaza ushirika wetu.Niwashukuru sana watu wa Dodoma kwenye jukwaa ili lengo letu ni tuweze kuinua uchumi,”amesema Mwenyekiti huyo.
Amesema michezo itawasaidia kuimarisha afya pamoja na kuendelea kuwavuta watu wengine kwa ajili ya kuutangaza ushirika.
Kwa upande wake, Mrajis Msaidizi Mkoa wa Dodoma,Joseph Chitinka amesema wameshiriki bonanza hilo kama familia na wamelifurahia kwa jinsi lilivyokuwa na ubora.
Chitinka ametoa wito kwa vyama vingine kujiunga katika umoja huo kwani kuna fursa nyingi ambazo watakutana nazo.
“Vipo vyama mawilayani na hapa mkoani vinatakiwa kuchangamkia fursa jukwaa la ushirika kwani Kuna fursa nyingi ambazo watakutana nazo,”amesema Chitinka


Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dodoma,Ibrahim Sumbe,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Bonanza la Ushirika kuelekea Siku ya kuelekea Jukwa la Ushirika Mkoa wa Dodoma linalotarajia kufanyika Mei 15-16,mwaka huu katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Bonanza lililofanyika leo Mei 10,2025 katika Viwanja wa Kilimani Jijini Dodoma.


Mrajis Msaidizi Mkoa wa Dodoma,Joseph Chitinka,akielezea lengo la Bonanza hilo kuelekea Siku ya kuelekea Jukwa la Ushirika Mkoa wa Dodoma linalotarajia kufanyika Mei 15-16,mwaka huu katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Bonanza lililofanyika leo Mei 10,2025 katika Viwanja wa Kilimani Jijini Dodoma.





























Wanaushirika wakishiriki michezo mbalimbali wakati wa Bonanza lililofanyika leo Mei 10,2025 katika Viwanja wa Kilimani Jijini Dodoma kuelekea Jukwa la Ushirika Mkoa wa Dodoma linalotarajia kufanyika Mei 15-16,mwaka huu katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)