MBUNGE wa Tunduru Kaskazini (CCM) Mhe.Hassan Zidadu,akichangia leo Mei 9,2025 bungeni Dodoma mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025-2026.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MBUNGE wa Tunduru Kaskazini,Hassan Zidadu (CCM) amemshukuru Waziri wa Maji,Jumaa Aweso kwa kumaliza tatizo la Maji Tunduru Kaskazini kwani wakazi wa maeneo hayo walikuwa wakipata shida.
Mhe.Zidadu ametoa shukrani hizo leo Mei 9,2025 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bungeni mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025-2026.
Zidadu amesema awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jimbo hilo lakini alipofika Aweso alilimaliza kwa kutoa Sh milioni 500.
“Waziri wa Maji nilipokuita ulikuja na palepale alichukua hatua katika kikao cha Baraza la Madiwani,tunakushukuru sana sana kwani ulitupa milioni 500 pamoja na kusaidia kupata pikipiki kwa ajili ya kuwawezesha wataalamu,”amesema