Featured Kitaifa

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA MAJI KWA KISHINDO

Written by mzalendoeditor
BUNGE limepitisha bajeti ya Shilingi trilioni 1.01 ya  Wizara ya Maji kwa huku Waziri wa Wizara hiyo Juma Aweso akiwashukuru Wabunge kwa michango yao ambapo ameahidi kujibu hoja zao kwa njia ya maandishi.
Akihitimisha kwa kifupi Aweso amesema: “Kubwa ninalotaka kusema mmechangia ninawashukuru niwaahidi kila Mbunge ambaye amechangia nitamjibu kwa maandishi.Nitumie nafasi hii kumpongeza Rais Dk Samia hakuna hata mmoja asiyejua mazuri ya Rais”
Wabunge wakichangia katika bajeti hiyo wameiomba Wizara ya Maji kupeleka fedha kwa wakati kwa wakandari ambao wamekuwa wakitekeleza miradi ya maji,wataalamu wa maji kusoma  katika Chuo cha Maji ili utaalamu waupeleke katika maeneo mengine,waboreshe  upatikanaji wa maji,na upatikanaji wa vifaa

About the author

mzalendoeditor