Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .
…
WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Jumla ya miradi ya maji 2,331 imekamilika ambapo 1,965 ni ya vijijini na 366 ni ya mijini .
Hayo yameelezwa leo Mei 8,2025 na Mhe.Aweso wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Amesema kuwa kukamilika kwa miradi hivyo kumeboresha upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 83 mwezi Desemba, 2024 na maeneo ya mijini kutoka wastani wa asilimia 84 hadi asilimia 91.6.
Aidha amesema kuwa kuanzishwa kwa RUWASA kumejenga miradi 3,379, na kupeleka huduma ya maji katika vijiji 10,517 kati ya vijiji zaidi ya 12,318. RUWASA imefanya mapinduzi makubwa katika kujenga na kuboresha huduma ya maji vijijini.
“Baadhi ya miradi iliyokamilika ni awamu ya kwanza ya mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kunakuwa na Gridi ya Taifa ya Maji (National Water Grid) wa miji ya Kahama, Shinyanga, Tinde, Nzega, Tabora, Igunga mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Dodoma unaendelea.”amesema Mhe.Aweso
“Kuanza kwa utekelezaji wa miradi ya maji ya kimkakati ikiwemo mradi wa maji wa miji 28,mradi wa bwawa la Farkwa, mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi Simiyu; mradi wa maji kutoka Kahama kwenda Halmashauri ya Ushetu; mradi wa kutoa maji Dambia kwenda Haydom; mradi wa maji Ukirigulu, Koromije hadi Sumve; na mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji na utunzaji wa mazingira Jijini Tanga pamoja na miji ya Muheza, Pangani na Mkinga. “amesema
Pia Kuimarika kwa uhusiano na ushirikiano na wadau wa maendeleo hivyo, kuongeza wigo wa upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi pamoja na ushauri wa kitaalam.