Featured Kitaifa

HISTORIA YA AWESO SEKTA YA MAJI YAZIDI KUNG’ARA UPATIKANAJI WA MAJI VIJIJINI ASILIMIA 83,MIJINI  91.6

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .
……
Waziri wa Maji Juma Aweso amesema upatikanaji wa Maji kwa Sasa ni asilimia 83 katika maeneo ya vijijini na 91.6 mijini.
Kauli hiyo ameitoa Leo bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na matumizi kwa Wizara hiyo katika bajeti ya mwaka 2025-2026.
Waziri Aweso amesema upatikanaji wa vjijini kwa Sasa ni asilimia 83 ikilinganishwa na asilimia 76 miaka kadhaa iliyopita.
Waziri Aweso amesema  lengo la Serikali ni kuhakikisha zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa vijijini wanapata maji safi na salama.
Kwa upande wa mijini upatikanaji wa Maji kwa Sasa ni asilimia 91.6 lengo likiwa ni kufikia asilimia 95

About the author

mzalendoeditor