Featured Kitaifa

WIZARA YA MADINI YAOMBA KUIDHINISHIWA BILIONI 224.

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Madini,Anthony Mavunde bungeni  wakati akiwasilisha hotuba ya  bajeti ya Wizara hiyo leo Mei 2,2025 bungeni jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

…….

Wizara ya Madini imeliomba Bunge kuridhia na kupitisha makadirio ya bajeti ya Shilingi Bilioni 224,984,150,000.00 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 huku itaja Vipaumbele mbalimbali ikiwemo  kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli.

Akiwasilisha  leo Mei 2,2025 bungeni na Waziri wa Madini,Anthony Mavunde,amesema  Serikali inaendelea kuchukua hatua za kimkakati ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje katika sekta ya Madini nchini ili kuongeza thamani ya Madini hayo.
Aidha Mavunde amevitaja vipaumbele vingine ni  kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa,kuendeleza mnyororo wa thamani katika madini muhimu na madini mkakati.
“Kuhamasisha uwekezaji na uongezaji thamani madini,kuimarisha uendeshaji wa minada na maonesho ya madini ya vito,kuongeza uwekezaji kwenye tafiti za madini za kina, kurasimisha”amesema Mavunde
Vipaumbele vingine ni kuendeleza wachimbaji wadogo wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu  na kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya wizara ya madini.
Pia amesema kuwa  shilingi bilioni 124,604,788,000.00 sawa na asilimia 55.38 ya bajeti yote ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 100,379,362,000.00 sawa na asilimia 44.62 ya bajeti yote ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 24,268,585,000.00 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi (PE) na shilingi bilioni 76,110,777,000.00 kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC) ya Wizara na Taasisi zilizo chini yake

About the author

mzalendoeditor