Wananchi
wa Kata ya Kihesa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa
wakikagua majina yao katika daftari la awali la wapiga Kura lililobandikwa
katika kiuo cha kujiandikishia wapiga Kura kilichopo ofisi ya Mtendaji Kihesa.
Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi imeanza awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari
la Wapiga Kura katika mikoa 15 ya Tanzania bara kuanzia Mei Mosi hadi 07, 2025
unaokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali.

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele
akitembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
awamu ya pili mkoani Njombe linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa daftari la
awali la wapiga kura ambapo mikoa 15 imeanza zoezi hilo litafanyika kwa siku
saba kuanzia Mei 1 hadi 7, 2025.

Na. Mwandishi wetu, Iringa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka
wananchi kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara inayotekeleza mzunguko wa
kwanza katika awamu ya pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga
Kura kujitokeza katika vituo walivyojiandikishia na kutazama daftari la awali
lilolowrekwa wazi na kutoa taarifa za wale waliokosa sifa kuwepo kwenye daftari
hilo.
Akizungumza baada ya kutembelea vituo katika
Halmashauri za Manispaa ya Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Halmashauri
ya Mji wa Mafinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, Mwenyekiti
wa TumeHuru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema
wananchi wameonesha mwitikio katika siku ya kwanza ya zoezi hilo la siku saba
na kuwataka kuhakiki taarifa zao.
Jaji Mwambegele amesema Tume imeweka wazi daftari
la awali la wapiga kura katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha na
kuboresha taarifa za Wapiga kura katika awamu ya kwanza, hivyo wananchi
wajitokeze kuhakiki taarifa zao na kutoa taarifa za wale ambao hawastahili
kuwepo katika Daftari hilo.
“Nawasihi wananchi endapo wataona katika
Daftari ambalo tumeliweka katika kila kituo kuna mwananchi ambaye amekosa sifa kama
vile kufariki basi wawe huru kwa kutumia fomu namba 5B kumuondoa huyo ambaye
amekosa sifa za kuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.”alisema.
Aidha, amesema yeye pamoja na viongozi
wengine wa Tume wakiwepo Wajumbe wa Tume wametembelea mikoa yote inayotekeleza zoezi
hilo na kushuhudia mwitikio wa watu vituoni, huku vituo vikifunguliwa kwa
wakati uliopangwa wa saa 2:00 asubuhi.
“Wananchi wamejitokeza vizuri kuja kuboresha taarifa
zao wale ambao hawakuboresha taarifa zao katika awamu ya kwanza ya uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,”alisema Jaji Mwambegele.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya pili unafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la
Wapiga Kura kuanzia Mei 01, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai, 2025.
Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa
mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa
pili mikao 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya
mafunzo.
Mikoa itakayohusika kwenye mzunguko wa kwanza
wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza,
Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo
zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 1 hadi 7 mwaka huu.
Aidha, mzunguko wa pili utahusisha mikoa ya
Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es
Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja,
Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16
hadi 22, 2025.
Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa
Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na
vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja
na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia Juni 28 hadi Julai 04, 2025.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya
jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo
7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.
Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga
kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa
zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za
kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
Mambo mengine ni kuhamisha taarifa za wapiga
kura waliohama kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za
kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni
kutoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura
na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao
hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25
Machi, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na baadhi ya vijana waliojitokeza kujiandikisha kwa mara ya kwanza katika moja ya vituo Mkoani Iringa.
Matukio mbalimbali ya ziara ya Mwenbyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakati akitembelea vituo mkoani Iringa