Featured Kitaifa

WIZARA YA ELIMU NA WADAU WAJADILI UTEKELEZAJI SAMIA SCHOLARSHIP 360 EXTENDED DSP KWA WANAFUNZI WA SAYANSI

Written by mzalendoeditor

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na wadau zikiwemo taasisi zilizo chini yake, wamekutana jijini Dodoma tarehe 26 Aprili kujadili namna ya kuanzisha na kutekeleza Programu ya *Samia Scholarship 360 extended DSP*. Programu ambayo inalenga kutoa ufadhili kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na kufaulu vizuri katika masomo ya sayansi ili kusomea Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili katika fani ya sayansi ya data kwenye vyuo mbalimbali nje ya nchi.

Kikao hicho kimeongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, ambapo Waziri amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika utekelezaji wake ili kuhakikisha program inakuwa endelevu na kufanikisha malengo ya kuwajengea vijana umahiri na ujuzi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya taifa.

Aidha, Prof. Mkenda ameongeza kuwa ni muhimu kutangaza mapema fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo katika ngazi tofauti za elimu ili kuwasaidia wanafunzi wenye sifa stahiki kupata nafasi na kunufaika na programu kama hii.

About the author

mzalendoeditor