Featured Kitaifa

WAZIRI MASAUNI AZINDUA BODI MPYA YA NEMC

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati akizindua Bodi ya tisa ya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dodoma Aprili 15, 2025, ambapo Mha. Mwanasha Tumbo ndiye Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akimkabidhi nyaraka mbalimbali Mwenyekiti wa Bodi ya tisa ya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mha. Mwanasha Tumbo mara baada ya kuizindua Bodi hiyo, Dodoma Aprili 15, 2025.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tisa ya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), uzinduzi huo umefanyika Dodoma Aprili 15, 2025 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mha. Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tisa ya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), uzinduzi huo umefanyika Dodoma Aprili 15, 2025 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya tisa ya Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kuizindua, Dodoma Aprili 15, 2025.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mha. Hamad Masauni ameielekeza Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kulisimamia kikamilifu baraza hilo ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira nchini.
Mha. Masauni ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma Aprili 15,2025 wakati akizindua bodi hiyo na kuongeza kuwa ihakikishe inatafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazosababisha uchafuzi wa mazingira nchni.
“Lingine pia ni uhamasishaji na elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwani wananchi bado hawana elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira, ili ushiriki katika shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira kama ukataji wa miti ovyo, uchomaji misitu na utupaji taka hovyo,”amesema.
Sambamba na hayo ameongeza kuwa bodi hiyo inapaswa kushirikiana na Wizara pamoja na NEMC katika mchakato wa marekebisho ya sheria ya usimamizi wa Mazingira Sura Na 191 inayolenga kuimarisha baraza hilo katika usimamizi wa mazingira.
“Pia, mwendelee kubuni na kuandaa mikakati ya kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi kama ilivyochambuliwa katika mikataba ya kimataifa na katika eneo hilo hilo, kuongezeka kwa joto miale, kupungua kwa mvua na mvua zisizo tabirika na majanga mengine yanayochangia kuharibika kwa mazingira,” ameongeza.
Kwa upande wake Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis Hamza Khamis amesema kuwa kwasasa wanataka kuitoa NEMC kwenda kuwa neema kwasababu wamejifunza na kuona mazingira ya tofauti kwani Zanzibar tayari wana ZEEMA.
“NEMC hii iende kuwa mamlaka ambayo tutakuwa tuna nguvu na makucha zaidi ya kufanya kazi zetu, tunafika wakati tunatumia sharia zetu lakini zinakuja zinagonga inabidi sasa wengine waje wanatumia sharia zao lakini sasa kwasababu tutaitengeneza sasa itakuwa na nguvu mambo yatakwenda vizuri,” amesema.
Amesema walikuwa na baadhi ya changomoto ndogo ndogo ikiwemo uchafuzi wa mazingira hivyo wao baada ya kuja wataenda kuunganisha nguvu ya pamoja ili wakazitatue.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Cyprian Luhemeja amsema matarajio ya Rais ni kuona NEMC inayoweza kusiamamia mazingira vyema na yanalindwa hivyo anaamini utumishi utaonekana.

About the author

mzalendoeditor