Featured Kitaifa

BARRICK YADHAMINI KONGAMANO LA WANAFUNZI VYUO VIKUU LILILOFANYIKA CHUO KIKUU DODOMA

Written by mzalendoeditor

Afisa Raslimali Mwandamizi wa Barrick nchini,Chrispin Ngwaji akiwaeleza wanafunzi wa vyuo vikuu shughuli za kampuni ya Barrick nchini.
Mkuu wa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Joachim Nyingo akiongea katika kongamano hilo.
Mtendaji Mkuu wa AIESEC nchini,Vicent Manila
 
****
Katika kufanikisha dhamira yake ya uwezeshaji wa vijana,kampuni ya Barrick nchini imedhamini kongamano la vijana kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania, ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati wanapata fursa ya kuunganishwa pamoja na kujengewa uwezo katika masuala ya kuhimili soko la ajira,mbinu za kujiajiri na jinsi ya kukabiliana na ushindani wa fursa mbalimbali zinazojitokeza katika ulimwengu wa sasa wenye mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia.
Katika kongamano la AIESEC lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wanafunzi waliweza kujengewa uwezo katika masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick waliobobea katika fani mbalimbali na wadau kutoka taasisi nyingine waliodhamini na kushiriki.
Maofisa wa Barrick wakiongea na wanafunzi
Wanafunzi wakifuatilia mada zilizotolewa na wataalamu mbalimbali
Wanafunzi wakifuatilia mada zilizotolewa na wataalamu mbalimbali
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick walioshiriki katika kongamano hilo

About the author

mzalendoeditor