SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gassima Nyamo-Hanga pamoja na dereva wake Muhajir Mohamed Haule.
Marehemu Nyamo-Hanga na dereva wake wamefariki usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Aprili, 2025 katika ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.
Rais Dkt. Samia anawapa pole Wizara ya Nishati, TANESCO, familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Nyamo-Hanga na Haule.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu Nyamo-Hanga na Haule mahala pema peponi, Amina.
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu