Featured Kitaifa

ZAIDI YA ASILIMIA 70 FEDHA ZA MRADI WA HEET ZIMEELEKEZWA KATIKA UJENZI NA UKARABATI MIUNDOMBINU YA ELIMU YA JUU NCHINI

Written by mzalendoeditor

Zaidi ya asilimia 70 ya fedha za Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ya Fedha (HEET) zimeelekezwa katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu ya juu nchini.

Akizungumza kwa njia ya mtandao Aprili 2, 2025 katika kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wajumbe kutoka Benki ya Dunia, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa mpaka sasa mikataba ya ujenzi yenye thamani ya dola za Kimarekani zaidi ya milioni 333 imeingiwa na kazi inaendelea.

Ameongeza kuwa wizara imefanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na timu ya Benki ya Dunia iliyofanya mapitio ya utekelezaji wa mradi mwaka jana na kuleta matokeo chanya katika utekelezaji wa mradi

Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe wa Benki ya Dunia,Prof. Roberta Malee amesema kuwa timu hiyo inafanya mapitio ya mradi (MTR) ili kuona utekelezaji na changamoto zilizoibuka katika maeneo mbalimbali.

Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unalenga kuongeza fursa za mafunzo elimu ya juu, kuimarisha mazingira ya kujifunza, kuboresha usimamizi.

About the author

mzalendoeditor