Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ANATAJIA KUWA MGENI RASMI  KONGAMANO LA KIMATAIFA LA eLEARNING AFRIKA MEI 2025

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Perof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandisha wa habari (hawapo pichani) leo  machi 29,2025  jijini Dodoma kuhusu  kongamano la kimataifa la earning Afrika linalotarajiwa kufanyika Mei 07 hadi 09, 2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

WAZIRI  wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Perof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandisha wa habari  leo  machi 29,2025  jijini Dodoma kuelekea  kongamano la kimataifa la earning Afrika linalotarajiwa kufanyika Mei 07 hadi 09, 2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

 

WAZIRI  wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Perof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandisha wa habari  leo  machi 29,2025  jijini Dodoma kuelekea  kongamano la kimataifa la earning Afrika linalotarajiwa kufanyika Mei 07 hadi 09, 2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la earning Afrika linalotarajiwa kufanyika Mei 07 hadi 09, 2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

WAZIRI  wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Perof.Adolf Mkenda,ameyasema hayo leo  machi 29,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kuwa kongamano hilo litakuwa mara ya pili kufanyika nchini.

Prof.Mkenda amesema kongamano hilo linalenga kuleta makundi mbalimbali kutoka zaidi ya nchi 65 za Afrika kwa ajili ya kujadili,kubadilishana uzoefu,kuhamasisha uwekezaji na kuazimia mipango ya pamoja ya kuchagiza matumizi ya Teknolojia za kidijitali katika sekta ya Elimu barani Afrika.

“Kongamano hilo linatarajia kuanza Mei 7,2025 na kuhitimishwa Mei 9 ,2025. Mgeni Rasmi katika hafla ya ufunguzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mgeni Rasmi katika  hafla ya kuhitimisha Kogamano hilo, Mei  9, 2025, anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.”amesema Prof.Mkenda 

Aidha amesema kuwa Kongamaono la 18 la elearning Afrika litafanyika katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini dar es salaam kuanzia mei 07 hadi 09 mwaka huu,tangu kuasisiwa kwake mwaka 2005 kongamano hili lishafanyika nchi 17 ikiwemo Tanzania.

“Tanzania lilifanyika mwaka 2021 hivyo mwaka huu litakuwa linafanyika kwa mara ya pili,kongamano hili linalenga kuwakutanisha wadau zaidi ya 1500 kutoka zaidi ya 65 barani Afrika”,amesema Prof.Mkenda

 Prof.Mkenda  amesema makundi hayo ya wadau yatajumuisha watunga sera,watoa maamuzi,wataalamu wa Elimu,wataalamu wa Teknolojia,watafiti,wabunifu,wafanya biashara,wawekezaji na wadau wa maendeleo.

Hata hivyo  amesema kongamano hilo litajumuisha mkutano wa mawaziri zaidi ya 50 kutoka nchi 49 barani Afrika utakao kuwa na lengo la kuazimia mikakati ya pamoja na kuandaa nguvu kazi mahiri katika kubuni, kuzalisha,na kuimalisha matumizi ya kidigitali.

“Kama wenyeji wa kongamano hili nchi yetu inatarajia kunufaika na fursa mbalimbali kutokana na kuwa mwenyeji wa kongamano hili ambapo tutabaini mikakati mpya hususani katika sekta ya Elimu”,amesema Prof.Mkenda 

Kongamano hilo litaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “kufikilia upya Elimu,na maendeleo ya raslimali watu kwa ustawi wa Afrika”

About the author

mzalendoeditor