Featured Kitaifa

TARURA YATOA SEMINA KWA JUMUIYA YA WANAHABARI MITANDAO YA KIJAMII TANZANIA (JUMIKITA)

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) leo tarehe 28 Machi, 2025 imefanya semina kwaajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Jumuiya ya Wanahabari Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ili waweze kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na TARURA na kuziandika kwa ufasaha kwa faida ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Moja ya mada ambayo iliyotolewa katika semina hiyo ni ujenzi wa madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ambayo ni ya gharama nafuu pia na inatoa fursa ya ajira kwa watanzania ambapo mada hiyo ilitolewa na Mhandisi Mshauri Pharles Ngeleja.

Aidha, mada nyingine ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Jamii Dkt. Heladius Makene iliyohusu Uhifadhi wa barabara na mitaro sio jalala.

About the author

mzalendo